Aug 17, 2018 16:12 UTC

Serikali ya Cameroon imesema kuwa, haitoifumbia macho mikanda ya video inayoenezwa katika mitandao ya kijamii ikiwaonyesha askari wa nchi hiyo wakiwanyanyasa na kuwaua wananchi.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuenea mikanda ya video ambayo inawaonyesha askari hao na bila ya huruma wakiwatesa na kisha kuwamiminia risasi raia kwa visingizio tofauti.

Rais Paul Biya wa Cameroon

Mashirika ya haki za binaadamu sambamba na kukemea vitendo hivyo, yameitaka serikali kuwachukulia hatua kali askari wanaohusishwa na jinai hizo.

Kwa maeneo zaidi tujiunge na mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati, Mosi Mwasi…………./

 

Maoni