Aug 17, 2018 16:13 UTC

Kiongozi wa Chuo cha Imam Swadiq (as) cha jijini Dar es Salaam, Tanzania Sheikh Hemed Jalala, ameonya tabia ya nchi za Kiafrika kuendelea kukumbatia mitaala na maelekezo ya nchi za kikoloni na kibeberu kwa kuwa mabeberu hao hawana nia njema na bara la Afrika.

Sheikh Jalala ameyasema hayo katika hotuba ya swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo jijini Dar es Salaam ambapo amekumbushia maneno ya thamani ya rais wa zamani wa Iran, Akbar Hashemi Rafsanjani wakati alipozitembelea nchi za Kiafrika ambapo alitoa mwito akizitaka nchi mabeberu zilizohusika na ukoloni, kulipa fidia kwa nchi wahanga kutokana na jinai zao kubwa walizozitenda barani humo.

Licha ya ulimwengu kuendelea, lakini bado athari ya ukoloni zinaendelea kuwatafuna Waafrika na kujikuta wakiendelea kufanywa watumwa

Kwa mujibu wa Sheikh Jalala, athari mbaya za ukoloni bado zimeendelea kuzididimiza nchi za bara la Afrika kutokana wakoloni wanakusudia kuyaona mataifa ya Kiafrika yakiendelea kuwa duni ili yaendelee kuwa tegemezi kwao.

Utumwa uliofanywa na wakoloni wenye mioyo ya kinyama

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam, Ammar Dachi kwa taarifa kamili………./

 

Tags

Maoni