Aug 25, 2018 14:45 UTC

Viongozi wa vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameijia juu Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo (CENI) kwa hatua yake ya kukata majina sita miongoni mwa majina ya waliojiandikisha kugombea kiti cha urais katika uchaguzi ujao nchini humo.

Kwa mujibu wa viongozi hao wa upinzani, panga hilo la kukata majina yao limesukummwa na sababu za kisiasa tu na hivyo wametishia kwenda mahakamani kuiburuza Tume hiyo ya Uchaguzi (CENI) .

Jean-Pierre Bemba, mmoja wa viongozi wa upinzani ambaye amezuiwa kugombea 

Miongoni mwa wapinzani mashuhuri ambao jinao lao limekumbwa na panga CENI, ni Jean-Pierre Bemba ambaye sasa hatoweza kushiriki kinyang'anyiro hicho.

Jengo la Tume hiyo ya Uchaguzi (CENI)

Kwa maelezo zaidi tujiunge na mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati Mosi Mwasi……………/

 

Tags

Maoni