Aug 30, 2018 16:59 UTC

Nchi za Africa Kusini na Rwanda zimekubaliana kushirikiana katika nyanja mbalimbali zikiwemo za uongozi bora na mipango ya maendeleo.

Haya yamesemwa na Waziri katika Ofisi ya Rais Nchini Afrika Kusini Anayehusika na Mipango ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Dr Nkosazana Dlamin Zuma anayeizuru Rwanda.

Rais Paul Kagame wa Rwanda

Kwa mujibu wa Bi Dlamin Zuma, mataifa ya Afrika yanatakiwa kuiga kasi ya maendeleo ya Rwanda licha ya nchi hiyo kukumbwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi…………/

Maoni