Aug 30, 2018 16:59 UTC

Baada ya Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi kusaini sheria inayopiga marufuku matumizi na biashara ya mifuko ya plastik nchini humo, wananchi wamekuwa wakihimizwa kuachana na matumizi ya mifuko ya aina hiyo ambayo inaharibu mazingira kwa kiasi kikubwa.

Hayo yanajiri katika hali ambayo Waziri wa Biashara wa nchi hiyo amekuwa akitembelea viwanda na mashirika yanayotengeneza mifuko ya karatasi inao zingatia mazingira sambamba na kuyashajiisha katika uwanja huo.

Matumizi ya mifuko inachafua mazingira

Hata hivyo kwa upande wao, wananchi wameitaka serikali kuhakikisha mifuko ya karatasi inapatikana kwa wingi kabla ya mifuko ya plastiki kutoweka katika matumizi. 

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura, Hamisa Issa kwa taarifa kamili………/

 

Tags

Maoni