Aug 30, 2018 17:00 UTC

Balozi wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania, Mousa Farhang, amesema kuwa, Sikukuu ya Ghadir sio kwa ajili ya Waislamu wa Shia pekee, bali Waislamu wa madhehebu yote duniani.

Farhang ameyasema hayo katika maadhimisho ya sherere ya sikukuu hiyo imefanyika katika Chuo Kikuu cha Jamiatul-Muustwafa cha mjini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine amewataka Waislamu kuwa macho mbele wa wafuasi wa kundi la Uwahabi ambalo ndilo chanzo cha ugaidi duniani.

Mousa Farhang, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania kulia

Katika sherehe hizo Kiongozi wa Chuo cha Imam Swadiq (as) cha jijini Dar es Salaam, Sheikh Hemed Jalala amelitaja tukio la Ghadir kuwa lenye mafungamano na maumbile ya mwanadamu ambaye daima anahitajia kuwa na kiongozi maishani mwake.

Kwa maelezo zaidi tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam, Ammar Dachi…………/

 

Tags

Maoni