Sep 02, 2018 02:23 UTC
  • Askari 30 wauawa na makumi wajeruhiwa katika shambulio la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria

Askari 30 wa Nigeria wameuliwa katika shambulio lililofanywa na magaidi wa kundi la Boko Haram dhidi ya kambi moja ya jeshi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Duru za jeshi la Nigeria zimetangaza kuwa makumi ya askari wengine ambao idadi yao bado haijafahamika sawasawa wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Tarehe 18 ya mwezi uliopita wa Agosti magaidi wa kundi hilo walishambulia pia maeneo kadhaa ya kaskazini mashariki mwa Nigeria na kusababisha maafa na hasara kubwa ya roho na mali kwa wakazi wa vijiji vya maeneo hayo.

Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani mashambulio na hujuma za kundi la kigaidi la Boko Haram na kutaka kuchukuliwa hatua za haraka za kuwatambua, kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wahusika wa jinai hizo.

Kundi la kigaidi la Boko Haram lilianzisha uasi, hujuma na mashambulio mwaka 2009 ngome yake kuu ikiwa katika eneo la kaskazini mwa Nigeria. Watu zaidi ya elfu 20 wameuliwa nchini humo na katika baadhi ya nchi jirani na zaidi ya milioni mbili na laki sita wamelazimika kuyahama makazi yao na kuwa wakimbizi kutokana na hujuma za kundi hilo.../

Tags

Maoni