Sep 04, 2018 13:51 UTC
  • Upinzani nchini Tanzania wapinga wakurugenzi wa Tume ya uchaguzi NEC kuwa wanachama wa CCM

Wabunge wa upinzani nchini Tanzania wamelalamikia hatua ya wajumbe na wasimamizi wa uchaguzi kutoka Tume ya Uchaguzi (NEC) kuwa wanachama wa chama tawala CCM.

Akihoji bungeni leo sababu ya wajumbe hao kuendelea kuhudumu katika tume hiyo licha ya kufahamika itikadi zao za kisiasa, mbunge wa Serengeti (Chadema) Chacha Marwa amesema kuwa, Tume ya Uchaguzi (NEC) haiwezi kuwa huru kwa kuwa wakurugenzi ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi, bado ni wanachama wa CCM kwa kuwa bado hawajawahi kujivua uanachama wa chama hicho. Aidha ameongeza kwamba, kwa mujibu wa Katiba afisa wa NEC hapaswi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini kile kinachoshuhudiwa hii leo ni kinyume. “Lakini wakurugenzi wengi wa NEC ni wanachama wa CCM, wengi waligombea ubunge.

Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania NEC

Walioshindwa wameteuliwa lakini hawajajiuzulu ubunge.“ Amesema mbunge huyo. Katika sehemu nyingine amezungumzia vitendo vya utekaji nyara dhidi ya wapinzani na kusema, walinzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) maarufu Green Guard wamekuwa wakiwateka wapinzani wakati wa mikutano ya kampeni, na kwamba hata yeye mwenyewe amewahi kukumbwa na jambo hilo. “Hivi ndio tume huru ya uchaguzi? Huku tunapoenda mnataka hadi damu imwagike?” Amehoji Marwa ambapo alikatizwa na Spika wa Bunge Job Ndugai. Ndugai amemueleza mbunge huyo kuwa maswali yake mawili yanatosha na kwamba anakoelekea anaweza kuzungumza kauli za kichochezi.

 

 

Tags

Maoni