Sep 09, 2018 02:47 UTC
  • Watu 28 waaga dunia na kujeruhiwa katika ajali ya barabarani Tanzania

Kwa akali watu 15 wamepoteza maisha na wengine 13 kujeruhiwa katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea katika mkoa wa Mbeya, kusini mwa Tanzania.

Walioshuhudia wanasema lori la kubeba viazi lilipoteza mwelekeo katika eneo la mteremko na kugonga magari matano katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia jana Jumamosi.

Duru za habari zimeripoti kuwa, ajali hiyo imehusisha matrela mawili ya kusafirisha mafuta ya petroli, malori mawili na mabasi mawili madogo ya abiria.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amesema, “Tumeshuhudia ajali nyingine, ambayo imesabisha wananchi wenzetu kupoteza maisha. Nimesikitishwa sana na maafa haya.” 

Ajali nyingine iliyotokea Tanzania miezi mitatu iliyopita

Katika siku za hivi karibuni Tanzania imekuwa ikikumbwa na ajali za barabarani na ambazo zimesababisha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha.

Mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, watu 14 walifariki dunia katika ajali nyingine mbaya ya barabarani iliyotokea katika mkoani Pwani nchini Tanzania.

Kutozingatia sheria za barabarani na madereva kuendesha magari kwa mwendo wa kasi kunatajwa kuwa sababu kuu za kukithiri ajali hizo. 

Tags

Maoni