Sep 10, 2018 06:12 UTC

Serikali ya Tanzania imesema, hadi kufikia sasa haijafahamika chanzo cha ugonjwa wa Lupa ulioikumba nchi hiyo.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ya nchi hiyo imesema, ingawa ugonjwa huo umeshaua mtu mmoja hadi hivi sasa na kesi za wengine kumi zikifuatiliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, lakini bado serikali haijatambua chanzo cha ugonjwa huo.

Taarifa kamili anayo mwandishi wetu Ammar Dachi

Tags

Maoni