Sep 11, 2018 06:14 UTC

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania, Bw. Musa Farhang amemzawadia Mufti wa nchi hiyo, Sheikh Abubakar bin Zubeir safari ya kuitembelea Iran yeye na familia yake.

Ahadi hiyo ameitoa katika hafla ya kumpongeza mheshimiwa Mufti Abubakar Zubeir iliyoandaliwa na Vijana wa Baraza la Waislamu Tanzania BAKWATA kwa kupeleka mbele baraza hilo katika kipindi cha utawala wake wa miaka mitatu.

Maelezo zaidi yamo katika ripoti ya mwandishi wetu Ammar Dachi kutoka Dar es Salaam.

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar bin Zubeir

 

Tags

Maoni