Sep 11, 2018 07:13 UTC
  • Kipindupindu chaua watu 16 katika mji mkuu wa Zimababwe, Harare

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Huduma za Afya na Tiba katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare amesema watu wasiopungua 16 wamefariki dunia wiki iliyopita kutokana na mripuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Clemens Dori ameashiria kuenea maambukizi ya kipindupindu kusini magharibi mwa Zimbabwe na kueleza kwamba watu 106 wamelazwa hopsitali ya maradhi ya maambukizi mjini Harare.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa Idara ya Huduma za Afya na Tiba katika mji wa Harare ameongeza kuwa maafisa husika wameweka usimamizi maalumu katika maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo na kutuma kwenye maeneo hayo timu za maafisa wa Wizara ya Afya za uchukuaji hatua za haraka.

Katika kipindi cha kati ya mwezi Agosti mwaka 2008 hadi Juni 2009 watu 98,596 walipatwa na ugonjwa wa kipindupindu nchini Zimbabwe ambapo 4,369 miongoni mwao waliaga dunia kutokana na athari za maambukizi ya ugonjwa huo.../

Tags

Maoni