Sep 12, 2018 03:53 UTC
  • Zimbabwe yatangaza hali ya hatari baada ya kuzuka kipindupindu katika mji mkuu Harare

Serikali ya Zimbabwe imetangaza hali ya hatari baada ya kuibuka maradhi ya kipindupindu katika mji mkuuu Harare.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, baada ya watu wasiopungua 20 kupoteza maisha hadi sasa kufuatia kuzuka maradhi ya kipindipundu mjini Harare, jana serikali ilichukkua uamuzi wa kutangaza hali ya hatari.

Ripoti za kiafya zinasema kuwa, zaidi ya watu 2,000 wamethibitishwa kwamba, wanauguua maradhi ya kipindupindu.

Uhaba wa maji safi na salama ya kunywa ni moja ya matatizo yanayoikabili Zimbabwe

Idara ya Manispaa ya jiji la Harare ambayo imekuwa ikipambana na maradhi ya kipindupindu kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, imetangaza kuwa, imechukua hatua za kukabiliana na maradhi hayo kama vile kuhakikisha wakazi wa jiji hilo wanapata maji safi na salama ya kunywa.

Clemence Duri, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Afya wa mji mkuu wa Zimbabwe, Harare ametangaza kuwa mlipuko wa magonjwa ya kipindupindu na homa ya matumbo umeua watu wasiopungua 20 katika jiji hilo katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Ugonjwa wa kipindupindu umekuwa ukitokea mara kwa mara katika vitongoji vya kandokando ya jiji la Harare ambako wakazi wake hawapati maji safi ya kunywa na huduma za afya. Maeneo hayo pia yanasumbuliwa na ukosefu wa miundombinu kutokana na kupuuzwa kwa miaka mingi.

Tags

Maoni