• Shule za Afrika Kusini kuanza kufunza Kiswahili

Waziri wa Elimu ya Msingi wa Afrika Kusini amesema shule za nchi hiyo zitaanza kufunza lugha ya Kiswahili kuanzia mwaka 2020.

Angie Motshekga aliyasema hayo jana Jumatatu na kufafanua kuwa, uamuzi huo wa kuanza kufunzwa lugha ya Kiswahili latika shule za umma, binafsi na huru za nchi hiyo umeidhinishwa na Baraza la Mawaziri la nchi hiyo.

Waziri huyo amebainisha kuwa, "Tunaamini kwamba, kufundishwa lugha ya Kiswalihi katika shule za Afrika Kusini kutasaidia kuimarisha utangamano wa kijamii na Waafrika wenzetu." 

Amesema Kiswahili kina uwezo wa kupanuka na kuenea katika nchi za Afrika ambazo hazizungumzi lugha hiyo, na kina uwezo wa kuwakurubisha tena pamoja wananchi wa Afrika.

Kinara wa chama cha upinzani cha EFF nchini Afrika Kusini, Julius Malema

Kiswahili ni lugha ya kwanza ya Kiafrika kutoka nje ya Afrika Kusini kufunzwa katika shule za nchi hiyo.

Mwezi uliopita, kinara wa upinzani nchini Afrika Kusini, Julius Malema alikitaja Kiswahili kama lugha ya aina yake ambayo inaweza kutumika katika nchi zote za bara Afrika, kama njia moja ya kuliondoa bara hilo kutoka katika minyororo ya ukoloni mambo leo.

Tags

Sep 18, 2018 07:17 UTC
Maoni