Sep 22, 2018 03:11 UTC
  • Polisi Nigeria wawashambulia kwa risasi Waislamu katika maombolezo ya Ashura

Polisi nchini Nigeria wamewafyatulia risasi Waislamu waliokuwa katika maomboleza ya ashura na kujeruhi baadhi yao.

Televisheni ya al Alam imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, katika hali ambayo miji mbalimbali ya Nigeria siku ya Alkhamisi ilishuhudia maadhimisho makubwa ya kukumbuka siku alipouawa shahidi Imam Husain AS, wanajeshi wa Nigeria waliweka ulinzi mkali pembeni mwa maadhimisho hayo na katika baadhi ya maeneo wamewashambulia kwa risasi Waislamu waliokuwa katika maombolezo.

Maadhimisho ya Muharram nchini Nigeria

 

Jeshi la polisi mjini Zaria limewatupia mabomu ya kutoa machozi Waislamu hao mbali na kuwafyatulia risasi na kujeruhi Waislamu kadhaa.

Katika mji mkuu Abuja pia, polisi na wanajeshi wa Nigeria wametoa vitisho kwa Waislamu na kuwatia mbaroni Waislamu wengi.

Katika mji wa Jussi pia, jeshi la Nigeria limejaribu kuwatawanya Waislamu waliokuwa katika maomboleza ya Ashura ya Imam Husain AS na kuzuia misafara yao ya maombolezo.

Tags

Maoni