Sep 22, 2018 16:34 UTC

Waziri wa Usalama nchini Uganda Jenerali Elly Tumwine, amewataka waandishi wa habari kutumia vyema taaluma yao ili wasiitumbukize nchi hiyo katika machafuko.

Tumwine amesema kuwa, aghlabu ya waandishi wa habari wanalipwa na mashirika ya kigeni hususan ya nchi za Ulaya ambazo kwa mujibu wake, haziitakii mema Uganda.

Mwaandishi wa habari Uganda akiwa amepigwa risasi

Hayo yamekuja kufuatia malalamiko ya waandishi wa habari ambao wamekuwa wakilalamikia ukandamizaji wa kuchupa mipaka wa jeshi la polisi dhidi yao hasa katika uchaguzi mdogo uliopita.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Kampala, Kigozi Ismail kwa taarifa kamili………../

 

 

Tags

Maoni