Oct 16, 2018 17:59 UTC

Kufuatia hatua ya serikali ya Angola kuwatimua makumi ya maelfu ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa lengo la kutaka kusafisha sekta ya madini ya alimasi kutokana na uwepo wa Wakongomani, serikali ya Kinshasa imekasirishwa na suala hilo.

Kufuatia hatua hiyo serikali ya Kongo DR imeamua kuunda kamati ya kuchunguza suala hilo huku ikilaani kitendo cha serikali ya jirani yake huyo kuwaswaga kama wanyama raia wake.

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Hayo yanajiri kufuatia kuibuka tuhuma mbalimbali kwamba askari wa Angola mbali na kuwaswaga Wakongomani hao, walifanya mauaji, uporaji ubakaji na vitendo vingine viovu.

Tujiunge na mwandishi wetu wa eneo la Afrika ya Kati Mosi Mwasi kwa taarifa kamili…………./

 

Tags

Maoni