Oct 16, 2018 18:03 UTC

Bunge la Rwanda limeanzisha zoezi la kuihoji tume ya taifa ya nchi hiyo inayoshughulikia faili la mauaji ya kimbari ya 1994, juu ya idadi kubwa ya watu waliokutikana na hatia ya mauaji hayo na kukwepa mkono wa sheria.

Hii ni baada ya tume ya kupambana na mauaji ya kimbari kulieleza bunge la Rwanda kwamba zaidi ya watu elfu kumi hawajulikani waliko baada ya kupatikana na hatia.

Kipindi cha kujiri mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994

Mbali na hayo ni kwamba mamia ya watu hao wanaishi katika nchi za nje kwa amani, licha ya kwamba walitambulika kuwa wahalifu.  
Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi………../

 

Tags

Maoni