Oct 16, 2018 18:32 UTC

Kufuatia ongezeko la talaka kati ya wanandoa katika jamii visiwani Zanzibar, Jumuiya ya Maimamu JUMAZA imezindua chuo cha maadili ya ndoa na mtaala wake ambacho kitakuwa na jukumu la kutoa mafunzo bora ili kupunguza ongezeko hilo.

Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Hassan Othman Ngwali, amepongeza ufunguzi wa chuo hicho huku akisema kuwa hiyo ni hatua muhimu kwa wale wote walioingia na wanaotaka kuingia katika ndoa kuweza kupata dira na mwongozo bora wa ndoa.

Ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kutokana na wanandoa kutofahamu misingi ya ndoa hiyo

Katika ufunguzi huo pia wazazi nao wamehimizwa kuwaelimisha watoto wao kuhusiana na suala zima la ndoa hususan katika kufahamu jukumu la baba baada ya kutolewa talaka.

 Tujiunge na mwandishi wetu wa visiwani Zanzibar, Harith Subeit kwa taarifa kamili……………./

 

 

Tags

Maoni