Nov 19, 2018 04:17 UTC
  • Algeria yaitolea wito Morocco kutatua hitilafu kati ya pande mbili

Rais wa Algeria amemtumia ujumbe Mfalme wa Moroccoa akitaka kupatiwa ufumbuzi hitilafu kati ya nchi mbili hizo na kuimarisha uhusiano wa pande mbili.

Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria jana Jumapili alimtumia ujumbe Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco akitaka kupatiwa ufumbuzi hitilafu kati ya nchi mbili hizo na akatoa mkono wa kheri na kupongeza kuwadia maadhimisho ya mwaka wa 63 wa uhuru wa Morocco.  

Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco
 

Mfalme Mohammed wa Sita wa Morocco hivi karibuni aliitolea wito Algeria kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na ya wazi na nchi yake ili kutatua hitilafu zilizopo. 

Mpaka kati ya Algeria na Morocco umefungwa tangu mwaka 1994 na nchi mbili hizo kwa mara ya mwisho ziliitisha kikao mwaka 2005. Wakati huo huo eneo la Sahara Magharibi linatajwa kuwa moja ya sababu kuu za kuwepo hitilafu kati ya Morocco na Algeria. Harakati ya Polisario pia ambayo ni taasisi ya kijeshi na kisiasa inapigania kuwa huru eneo la Sahara Magharibi tangu mwaka 1973. Harakati hiyo inaendesha mapambano dhidi ya serikali ya Morocco tangu mwaka 1976 ambapo wanajeshi wa Uhispania waliondoka katika eneo hilo. 

Mapigano kati ya serikali ya Morocco na harakati ya Polisario yalianza mwaka 1975 ambapo mwaka 1991 pande mbili hizo zilisaini makubaliano ya kusimamisha vita chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa. Algeria inaiunga mkono harakati ya Polisario katika mapambano yake na kuitambua Morocco kuwa inakalia kwa mabavu maeneo ya Sahara Magharibi.     

Maoni