Dec 14, 2018 07:45 UTC
  • UNCTAD yahimiza biashara mtandaoni Afrika

Afrika haitofikia malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs iwapo haitokumbatia fursa ya kuwekeza katika biashara ya mtandaoni.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi wakati wiki ya mkutano wa biashara mtandaoni (eCommerce) barani Afrika ikimalizika leo Ijumaa jijini Nairobi Kenya.

Akizungumza pembizoni mwa mwa mkutano huo, Dkt. Kituyi amesema, mkutano huo umeonesha wazi kuwa kuna watu wengi barani Afrika ambao wana ujuzi, nia na jitihada za kusukuma mbele Malengo Endelevu ya Maendeleo, SDGs kwa kutumia biashara mtandaoni ili kufanikisha ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu.

Rais Kenyatta akihutubu katika mkutano wa biasahra mtandano barani Afrika, Nairobi 11/12/2018

Amesema washiriki wa mkutano wa Nairobi wamekubaliana kuhusu mbinu za kuhimiza watu wa Afrika kutumia fursa za biashara mtandanoni kukuza uchumi, kupunguza umaskini, kubuni ajira na kuendeleza mapato ya Afrika na kupanua wigo wa masoko ya biashara mtandaoni.”

Mkutano huo wa biashara mtandaoni ni wa kwanza kabisa kuhusiana na bara la Afrika, kwa lengo la kutoa taarifa na kuliweka bara hilo katika mazingira ambayo linaweza kufaidika na biashara za mtandaoni. Akifungua mkutnao huo Jumanne wiki hii Rais wa  Kenya, Uhuru Kenyatta, alisema ili Afrika iweze kupata faida za biashara mtandaoni...“Sera zinapaswa kuwa zinaweka mazingira rafiki na hivyo ni muhimu kwa sekta hii kupewa umuhimu unaohitajika.

Tags

Maoni