Dec 15, 2018 14:40 UTC
  • Waziri Mpango: Misaada ya wafadhili kwa Tanzania imepungua, nchi inapitia kipindi kigumu

Waziri wa Fedha na Mipango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa, nchi hiyo inapita kwenye kipindi kigumu kutokana na wafadhili kupunguza misaada; na ile iliyobaki imekuwa na masharti yakiwamo ya kukubali ushoga.

Dk. Philp Mpango ametoa kauli hiyo mjini Dodoma alipokuwa akifunga mkutano kati ya wizara hiyo na watoa huduma za serikali katika kukusanya mapato. Waziri wa Fedha na Mipango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema wazi kuwa, misaada imeporomoka sana na hata ile iliyobaki ina masharti mengi ya ovyo.

Dakta Mpango amesema: “Mtakuwa mmesikia jinsi ambavyo sasa wanafika mahala, hata bila aibu, wanasema sisi tuvumilie ushoga, Mnakubali? Mnakubali niende kuomba hela ya nchi halafu kuchekelea ushoga ambao hata mbuzi hawafanyi?

Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania

Aidha Waziri Mpango alihoji kwa kusema, tukipeleka jeshi letu kudhibiti magendo, wanasema tunarudisha nyuma biashara ya usafirishaji hapa nchini. Inawezekana? Kwa hiyo ninachotaka kuwaambia ni nini? Marehemu Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere) alitufundisha kwamba tumepata uhuru wa bendera, lakini tuna kazi ya kutafuta uhuru wa kiuchumi,”

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Bunge la Umoja wa Ulaya limetoa njia iitakayo kwa mustakabali wao juu ya uhusiano kati yake na Tanzania kutokana kile walichokiita kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binaadamu nchini humo.

Bunge hilo limetaka kufanyika uchunguzi huru kuhusiana na malalamiko ya mashambulio na unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari, wapenzi wa jinsia moja, makundi ya watetezi wa haki za binadamu na wanasiasa wa vyama vya upinzani.

Maoni