Dec 16, 2018 07:43 UTC
  • Rais Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
    Rais Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Rais Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amemwachisha kazi waziri wake wa mambo ya nje, Charles Armel Doubane.

Shirika la habari la IRIB limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, baada ya kumwachisha kazi Charles Armel Doubane, Rais Touadéra amemteua Sylvie Baipo-Temon kushika nafasi hiyo.

Wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

 

Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati imesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na udhaifu wa kidiplomasia uliopo nchini humo na kwamba kwa kuteuliwa waziri mpya wa mambo ya nje, inatarajiwa kuwa harakati za kidiplomasia za nchi hiyo sasa zitaingia kasi. 

Doubane alishiriki pia katika sherehe za mwaka wa sitini wa Jamhuri Day za Jamhuri ya Afrika ya Kati zilizofanyika tarehe Mosi Disemba mjini Bangue.

Itakumbukwa kuwa, Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo ni miongoni mwa nchi masikini zaidi duniani, ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa mwaka 2013 baada ya kuondolewa madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo François Bozizé katika mashambulizi ya waasi wa Seleka.

Maoni