Apr 24, 2019 14:23 UTC
  • Kinara wa kundi la kigaidi la Al Shabab ajisalimisha kwa serikali ya Somalia

Idara ya taifa ya ujasusi ya Somalia (NISA) imesema kinara wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la al-Shabaab Aden Abdi, anayejulikana pia kama Aden Obe, ameliasi kundi la al-Shabaab na kujiunga na upande wa serikali.

Kwa mujibu wa NISA kinara hiyo amekuwa akiwasiliana kwa muda mrefu na NISA akitaka kujisalimisha. Afisa mwandamizi wa jeshi la serikali Ali Yakub Nur, amewaambia wanahabari kuwa NISA iliwasiliana na jeshi kutaka lishirikiane na  Abdi ili ajisalimishe.

Pia amesema aliiambia NISA kuwa alikuwa na ugomvi na kundi la al-Shabaab, na alikuwa tayari kujiunga na jeshi la serikali. Pia ameongeza kuwa alijisalimisha akiwa na mlinzi wake maalum, na wote sasa wako mikononi mwa majeshi ya serikali.

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia

Wanajeshi wa serikali ya Somalia wakishirikiana na askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika maarufu kama AMISOM wameimarisha vita dhidi ya magaidi wakufurishaji wa al-Shabab katika maeneo ya kati na kusini mwa Somalia ambapo wamefanikiwa katika kuwaangamiza magaidi wengi.

Tags

Maoni