Iran

 • Rais wa Iran asisitiza nafasi muhimu ya wanawake katika maendeleo ya jamii

  Jun 25, 2017 08:18

  Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza nafasi muhimu ya wanawake katika ustawi na maendeleo ya jamii sambamba na kusukuma mbele gurudumu la malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu.

 • Uwezo wa kijeshi wa Iran ni wa kuridhisha

  Jun 25, 2017 07:47

  Brigedia Jenerali Amir Ali Hajizadeh, Kamanda wa Jeshi la Anga za Karibu na Mbali la Walinzi wa Mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, SEPAH, amesema kuwa uwezo wa kijeshi wa hivi sasa wa Iran hauwezi kulinganishwa hata kidogo na wa kipindi cha vita vya miaka minene vya kujitetea kutakatifu na kuongeza kuwa hali hiyo ya kijeshi ni ya kuridhisha.

 • Kuaminiana pande mbili; sharti la kufanikiwa makubaliano ya nyuklia ya Iran na Magharibi

  Jun 25, 2017 03:58

  Ali Akbar Salehi Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran ameandika katika makala iliyochapishwa kwenye gazeti la The Guardian la nchini Uingereza kwamba, kufanikiwa makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi za Magharibi kunategemea ushirikiano na kiwango cha kuaminiana kati ya pande hizo na kwamba si kupitia siasa za kuvuruga mambo zinazofuatiliwa hivi sasa.

 • Iran yalaani njama za mashambulio ya kigaidi dhidi ya Msikiti wa Makkah

  Jun 24, 2017 14:07

  Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amelaani vikali njama chafu za kutekeleza mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Msikiti wa Makkah na kuwataka Waislamu kuwa macho na kufanya juhudi kubwa za kupambana na ugaidi.

 • Dakta Larijani: Israel ni mama wa ugaidi duniani

  Jun 24, 2017 03:40

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, katika kumbukumbu za karne za mwisho hakuna tukio baya kama la kuasisiwa utawala haramu wa Israel kwani kuanzishwa na kuundwa utawala huo kumepelekea kufanyika jinai ambazo hazijawahi kutokea katika historia.

 • Khatibu: Siku ya Kimataifa ya Quds imeiletea Iran heshima

  Jun 23, 2017 14:13

  Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesema kushiriki kwa wingi taifa la Iran katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, ni jambo ambalo limeuletea heshima na izza mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

 • Washiriki Siku ya Quds Iran waazimia kuunga mkono Palestina, wapinga mapatano na Israel

  Jun 23, 2017 14:05

  Washiriki wa maandamano ya mamilioni ya Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Iran wametoa taarifa na kutangaza kuunga mkono Intifadha au mwamko wa Palestina pamoja na mapambano ya Kiislamu huku wakibainisha upinzani wao kwa hatua za Saudi Arabia za kuelekea kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel.

 • Ujumbe wa mahudhurio ya mamilioni ya Wairani katika maandamano ya Siku ya Quds

  Jun 23, 2017 14:01

  Maandamano ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Quds yamefanyika katika hali tata zaidi ya matukio muhimu katika eneo la mashariki mwa Asia, ambapo mamilioni ya wananchi wa Iran katika pembe zote za nchi wameshiriki kwa hamasa katika maandamano hayo.

 • Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yaanza kote Iran

  Jun 23, 2017 07:57

  Maandamano ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds yameanza leo kote nchini Iran kwa kaulimbiu ya "Siku ya Kimataifa ya Quds; Nembo ya Umoja na Jihadi ya Umma wa Kiislamu, Uungajimkono kwa Wananchi Madhlumu wa Palestina na Kuangamizwa Utawala wa Kizayuni".