Mei 21, 2017 03:34 UTC
  • Rouhani: Washindi halisi katika uchaguzi wa Iran ni wananchi

Rais mteule wa watu wa Iran katika awamu ya 12 amesema mshindi halisi katika uchaguzi wa rais wa Mei 19 ni wananchi wa Iran.

Hassan Rouhani ambaye amepata ushindi katiak uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kiisalmu ya Iran na hivyo kumuwezesha kushikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha pili mfululizo siku ya Jumamosi amezungumza moja kwa moja kwa njia ya televisheni ya taifa na kusema: "Wananchi wameweka historia kwa kushirki kwa wingia wananchi katika  upigaji kura, pasina kujali ni nani waliyempigia kura. Hatua ya taifa la Iran kuniamini ni jambo linalopelekea nihisi mzigo mzito nilionao."

Rais mteule wa watu wa Iran aidha amemshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa uongozi wake wenye busara na hekima ambao umeweza kuliongoza taifa katika mawimbi makali ya uchaguzi na kulifikisha salama. Rais Rohani ameelezea matumaini kuwa atakuwa mwakilishi anayestahiki ili aweze kutekeleza matakwa ya taifa la Iran.

Wananchi Iran wakipiga kura katika uchaguzi wa rais

Aidha Rouhani amesema watu wa Iran katika ucahguzi wa rais wameonyesha azma yao ya kutaka kuimarisha uhusiano na dunia kwa msingi wa kuheshimiana na maslahi ya kitaifa. Aidha amesema uchaguzi wa Iran ni tangazo kwa nchi jirani na eneo kuwa, njia a kudhamini usalama wa eneo hili si kutegemea madola ya kigeni bali ni kuimarisha demokrasia na kueshimish kura za wananchi.

Tume uchaguzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, imemtangaza Rais Hassan Rouhani kuwa mshindi wa duru ya 12 ya uchaguzi wa rais iliyofanyika Ijumaakwa kupata kura milioni 23 ambazo ni sawa na asilimia 57.  Huku Sayyid Ibrahim Raeisi akishika nafasi ya pili kwa kupata kura milioni 15 ambayo ni sawa na asilimia 38.5. Viongozi mbali mbali duniani wanaendelea kumtumia Rais Rouhani asalamu za pongezi kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa rais.

Tags

Maoni