• Stratijia ya Marekani dhidi ya Iran imefeli

Mshauri wa ngazi za juu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, nguvu ya Marekani imo katika hali ya kusambaratika na kwamba, kuanzia mwaka 2025 na kuendelea nguvu itatoka katika ulimwengu wa Magharibi na kuhamia mashariki mwa dunia na barani Asia.

Meja Jenerali Yahya Rahim Safavi  ameashiria kushindwa stratejia ya marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuongeza kuwa,  hivi sasa Iran inatambulika kama nguvu ya kieneo katika eneo la magharibi mwa Asia.

Mshauri wa ngazi za juu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria kushindwa mtawalia mikakati ya Marekani kuanzia mwaka 2001 hadi sasa katika Mashariki ya Kati na kubainisha kwamba, Marekani ilifanya mashambulio ya kijeshi dhidi ya Afghanistan na Iraq na kugharamika kwa matrilioni ya dola ambapo mbali na kudhoofika, imelifanya dola hilo la kibeberu kushindwa kufikia malengo yake iliyokuwa imejiainishia.

Meja Jenerali Yahya Rahim Safavi, Mshauri wa ngazi za juu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Meja Jenerali Yahya Rahim Safavi amesema kuwa, hivi sasa muungano wa Marekani na Wazayuni, utawala wa Saudi Arabia, Uturuki na Jordan umeshindwa kufikia malengo yake huku muungano wa Iran, Russia, Syria na Hizbullah ya Lebanon ukiwa umepata ushindi na hivyo kuifanya Iran kuwa dola lenye nguvu katika eneo la Mashariki ya Kati.

Mshauri wa ngazi za juu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia njama za maadui za kuulenga usalama wa ndani na kubainisha kwamba, kuwekwa vikosi vya nchi kavu vya walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH katika mipaka ya mashariki lengo lake ni kuleta amani na uthabiti wa kudumu mashariki mwa nchi.

Jul 17, 2017 04:23 UTC
Maoni