• Larijani: Iran haitoinasa kwenye utando wa buibui wa Marekani

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema muamala wa wanasiasa wa Marekani ni wa kuvutia watu wa kawaida na wa mpito na akasisitiza kwa kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafuatilia kwa makini mienendo na hatua zao zote na itachukua uamuzi kulingana na maslahi yake ya taifa.

Ali Larijani ameyasema hayo leo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Saint Petersburg nchini Russia ambako atahudhuria kikao cha siku tano cha Umoja wa Mabunge Duniani kinachotazamiwa kuanza rasmi hapo kesho. 

Spika wa Bunge la Iran ameashiria msimamo unaotazamiwa kutangazwa na Rais Donald Trump wa Marekani kwamba Iran haijaheshimu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kueleza kwamba Iran haifurahishwi na mienendo ya kuvutia watu wa kawaida na ya mpito ya wanasiasa wa Marekani na wala haioni sababu pia ya kujiingiza kwenye utando wao wa buibui kwa sababu ya miamala yao hiyo.

Rais Donald Trump wa Marekani

Dakta Larijani ameeleza kuwa msimamo wa Trump utawadhuru Wamarekani na kuongeza kwamba hata viongozi wa nchi za Ulaya na nchi nyenginezo pia wamekemea muamala wa kiongozi huyo kuhusiana na JCPOA na kwamba hivi sasa imepatikana fursa nzuri kwa Iran ya kupiga hatua katika masuala mengine. 

Wataalamu na wachambuzi mbalimbali wanaeleza kuwa misimamo ya kiadui ya Marekani na mashinikizo yake dhidi ya Iran yanatokana na mafanikio ambayo Jamhuri ya Kiislamu imeyapata katika mapambano dhidi ya magaidi wanaosaidiwa na kuungwa mkono na Washington katika nchi za Iraq na Syria.../

Tags

Oct 13, 2017 08:00 UTC
Maoni