• Iran: Trump ni mfanyabiashara, hajui chochote kuhusu siasa na diplomasia

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Katika Masuala ya Kimataifa amesema tabia zisizo na mantiki za Rais Donald Trump wa Marekani zinaashiria kuwa hajui siasa wala hana ufahamu kuhusu mambo ya historia.

Ali Akbar Velayati amesema matamshi ya kijuba ya Trump yanaonyesha wazi kuwa hana ujuzi wowote katika masuala ya siasa na diplomasia na ni mtu ambaye amekulia katika ulimwengu wa biashara.

Amesema vikosi vyote vya jeshi la Iran likiwemo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC ni milki ya Wairani wote, ambavyo si tu vimeimarisha izza na usalama wa taifa, bali pia vimesimama kidete dhidi ya maaduia wa nchi hii sambamba na kuyapigisha magoti magenge ya kigaidi na kitakfiri na waungaji mkono wao. 

Rais Donald Trump wa Marekani

Dakta Velayati amesisitiza kuwa makubaliano ya JCPOA yalipasishwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na hivi sasa yanatambuliwa kuwa ya kimataifa. Ameongeza kuwa, wanachama wengine wa kundi la 5+1 wanapasa kuilazimisha Marekani isikengeuke fremu iliyoainishwa na wakala wa IAEA na mazungumzo  ya JCPOA. 

Siku ya IjumaaTrump alitoa matamshi yasiyo na msingi na kukariri tuhuma zisizo na maana za huko nyuma dhidi ya taifa la Iran; akidai kuwa Iran haijaonyesha moyo wa dhati katika kufungamana na makubaliano hayo ya nyuklia.

Aidha alikariri madai yake ya huko nyuma yasiyo ya kimantiki kwamba Tehran inaunga mkono ugaidi.

Tags

Oct 15, 2017 08:02 UTC
Maoni