• Shamkhani: Marekani, Uingereza na Saudia zapokezana mashambulizi ya Intaneti dhidi ya Iran

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kuwa, Marekani, Uingereza na Saudi Arabia zimeanzisha vita vya kupokezana katika Intaneti kuishambulia kila upande Jamhuri ya Kiislamu na taifa la Iran.

Ali Shamkhani amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya al Mayadeen ya Lebanon na kuongeza kuwa, matukio ya hivi karibuni nchini Iran yanaongozwa nchini Marekani na katika nchi waitifaki wake kama vile Uingereza na Saudia.

Ukandamizaji wa polisi nchini Marekani

 

Siku chache zilizopita, baadhi ya wananchi wa Iran walifanya mikusanyiko midogo midogo katika baadhi ya miji ya Iran kuilalamikia Serikali kutokana na kutelekezwa na taasisi za fedha na kupanda bei za baadhi ya bidhaa. Hata hivyo baadhi ya watu wachache waliokuwa wanasubiri tu fursa kama hiyo, walitumia kisingizio cha mikusanyiko hiyo kufanya fujo na kushambulia raia na maeneo ya umma katika baadhi ya maeneo nchini.

Ukatili wa Israel Palestina

 

Viongozi wa Marekani, utawala wa Kizayuni, utawala wa kiimla na kidikteta wa Aal Saud, UIngereza na vyombo vyao vya habari vilivyokuwa vinasubiri cheche ndogo tu vimetia chumvi kupindukia habari hiyo na kila leo vinazipa kipaumbele kikubwa habari zinazohusiana na matukio hayo.

Rais wa Marekani, Donald Trump amecharuka, kila leo anatumia mtandao wa Twitter kuchochea machafuko nchini Iran. Hata hivyo wananchi wanaoona mbali wa Iran jana walijitokeza kwa maelfu katika miji mbalimbali humu nchini kufanya maandamano ya kulaani machafuko na uchochezi unaofanywa na madola hayo ya kibeberu huku wakisema, Trump ambaye hakubaliki hata ndani ya Marekani kwenyewe kutokana na ukandamizaji wake, anapata uthubutu gani wa kusemea demokrasia imara ya nchini Iran. Au Saudi Arabia ambako maandamano ya namna yoyote ile yanahesabiwa kuwa ni jinai na usaliti, vipi haioni aibu kusemea demokrasia madhubuti ya Iran. Au nchi kama Uingereza ambayo kila leo kuna maandamano ya kulalamikia serikali na ukandamizaji wa polisi, vipi inajiingiza katika mambo ya ndani ya nchi nyingine?

Hivi ndivyo utawala wa kiimla wa Saudi Arabia unavyokandamiza maandamano ya wananchi. Unashamblia kikatili chochocte kilicho mbele yake

 

Tags

Jan 02, 2018 04:44 UTC
Maoni