• Iran: Kabla ya Trump kuingilia Iran, aokoe kwanza mamilioni ya Wamarekani wanaokufa njaa

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Uingereza amejibu uingiliaji wa Rais Donald Trump wa Marekani katika masuala ya ndani ya Iran na kusema kuwa, licha ya Marekni kujulikana kuwa na uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani, lakini kwa mwaka idadi kubwa ya raia wake huwa wanakufa njaa kutokana na tofauti ya kitabaka.

Hamid Baeidinejad ameongeza kuwa, kwa mujibu wa takwimu rasmi ikiwemo ripoti ya taasisi ya Feeding America ambayo inajishughulisha na utoaji misaada kwa watu masikini nchini humo, idadi ya Wamarekani wanaokabiliwa na hali mbaya ya njaa ni kubwa na ya kutisha.

Mmoja wa mamilioni ya Wamarekani wasio na makazi

Aidha balozi wa Iran nchini Uingereza amefafanua kuwa, takwimu hizo za kutisha zinaonyesha kwamba, watu milioni 42 wanakabiliwa na njaa kali ambapo kati yao milioni 13 ni watoto na zaidi ya milioni tano ni wazee. Balozi Hamid Baeidinejad amehoji kwamba, je, si ni vyema badala ya rais wa Marekani kushambulia mataifa mengine hususan Iran, kwanza atatue tatizo la Wamarekani wanaoangamia kwa njaa? Radiamali hiyo imekuja kufuatia matamshi mtawalia ya rais huyo wa Marekani kuchochea maandamano ya raia wa Iran katika baadhi ya miji humu nchini.

Hamid Baeidinejad, Balozi wa Iran nchini Uingereza

Kadhalika balozi wa Iran amegusia namna ambavyo serikali ya Washington imepuuza matatizo ya wakazi wa kisiwa cha Puerto Rico, ambao kwa muda wa miezi mitatu sasa wamekuwa hawana umeme kufuatiwa kukumbwa na kimbunga. Tangu Alkhamis iliyopita idadi ndogo ya raia wa Iran wamekuwa wakiandamana katika miji kadhaa sambamba na kupiga nara za kulalamikia ughali wa maisha na udhaifu katika usimamizi wa serikali, ambapo baadhi ya wahalifu wametumia vibaya maandamano hayo kufanya ghasia na uharibifu wa mali za umma.

Taasisi ambayo inajishughulisha na utoaji misaada kwa watu masikini nchini Marekani

Katika uwanja huo, Marekani, Israel na Saudia zimetangaza uungaji mkono wao kwa wafanya ghasia hao kwa lengo la kuibua machafuko nchini Iran. 

Tags

Jan 02, 2018 07:45 UTC
Maoni