• Propaganda chafu dhidi ya Tehran; ufunguo wa stratijia ya Marekani kuhusu Iran

Katika siku hizi Ikulu ya Rais wa Marekani, White House imeelekeza mazingatio na nguvu zake zote katika stratijia ya kutoa changamoto dhidi ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kati ya Iran na nchi za kundi la 5+1, masuala ya kikanda na maudhui ya haki za binadamu.

Katika mazungumzo yake ya Alkhamisi ya jana na mwenzake wa Ufaransa, Rais Donald Trump wa Marekani aliituhumu tena Iran kuwa inavuruga usalama eneo la Mashariki ya Kati. Vilivile White House ilitoa taarifa ikiituhumu Iran kwa kile ilichosema ni ukiukaji mkubwa wa haki za raia na kutangaza kuwa, serikali ya Marekani haitanyamaza kimya katika uwanja huo.

Msemaji wa White House, Sarah Sanders amesema, Trump anaamini kwamba, makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yana mapungufu mengi na kudai kuwa, serikali ya Marekani, Kongresi na washirika wake wanafanya jitihada za kuondoa mapungufu hayo.

Wakati huo huo Waziri wa Fedha wa Marekani, Steven Mnuchin amesema inatarajiwa kwamba, vitawekwa vikwazo vipya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Tangu miezi mitatu iliyopita yaani kuanzia tarehe 13 Oktoba mwaka jana, White House ilianza kutekeleza hatua mpya kupitia stratijia iliyobuniwa kwa kuzingatia madai ya kiuhasama na kiuadui ya siku zote ya serikali ya Washington. Stratijia hiyo inategemea masuala matatu makuu ambayo ni kufanya jitihada za kuvuruga makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, kutoa madai yasiyo na msingi kuhusu haki za binadamu na kudhihirisha uwezo wa makombora wa Iran kuwa ni tishio kwa usalama na amani. Hata hivyo serikali ya Donald Trump imefanya makosa mengi katika stratijia hiyo. Kwani hatua zisizo za kimantiki za Rais huyo wa Marekani sasa zimeifanya nchi hiyo ikabiliwe na changamoto ngumu.

Donald Trump

Trump anafanya njama za waziwazi za kuharibu kabisa mambo yote yaliyokusudiwa kuleta na kuimarisha amani ya kikanda na kimataifa katika mkataba wa nyuklia wa JCPOA. Si hayo tu bali kiongozi huyo wa Marekani pia anaendelea kukiuka makubaliano na sheria za kimataifa kama vile kuiondoa nchi hiyo katika makubaliano ya hali ya hewa, suala linaloifanya Marekani ikabiliane uso kwa uso na nchi za Ulaya, China na Russia. 

Kuhusu umuhimu wa kuheshimiwa makubaliano ya kimataifa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Dakta Muhammad Javad Zarif alisema jana baada ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya na Mawaziri wa Nje wa Ufaransa, Uingereza na Ujerumani kwamba: Umoja wa Ulaya na nchi hizo tatu zinajua vyema kwamba, sharti la Iran kuendelea kuheshimu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni wao pia kuheshimu na kutekeleza kikamilifu makubaliano hayo.  

Image Caption

Donald Trump ambaye nchi yake Marekani inatambuliwa kuwa mkiukaji mkubwa zaidi wa haki za binadamu, ameendelea kuziunga mkono na kuzisaidia tawala za shari na zinazoua watoto wadogo kama utawala haramu wa Israel na utawala wa kifalme wa Saudi Arabia ambao ameufanya kuwa n'gombe wake wa kukamua maziwa. Trump ameanzisha kile kinachoitwa muungano wa kimataifa wa eti kupambana na ugaidi kwa shabaha ya kuuza silaha za mabilioni ya dola kwa nchi kama Saudia. Ili kutimiza malengo yake ya kishetani, pia Donald Trump sasa ameanzisha muungano wa pande tatu za Washington, Tel Aviv na Riyadh zinazoshirikiana katika kupanga na kutekeleza njama za kutaka kuiangusha Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran.

Watoto wa Yemen, wahanga wa mashambulizi ya Saudia ikisaidiwa na Marekani na Israel

Mienendo kama hii haikubaliwi kabisa na jamii ya kimataifa, na Marekani inapaswa kuelewa kwamba, haiwezi tena kuwatwisha walimwengu matakwa na sera zake za kishetani.    

Jan 12, 2018 08:21 UTC
Maoni