Jan 13, 2018 14:18 UTC
  • Wizara ya Mambo ya Nje Iran yamjibu Trump, Tehran haitafanya mazungumzo kuhusu JCPOA

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa rasmi ikitangaza kuwa, kwa mara nyinghine tena Rais wa Marekani amelazimika kurefusha muda wa kusitisha vikwazo vya nyuklia vya Iran licha ya juhudi zake za mwaka mzima za kutaka kufuta makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Taarifa hiyo imesema kuwa, uimara wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na uungaji mkono wa kimataifa kwa makubaliano hayo vimefunga njia ya jitihada za Rais wa Marekani, utawala wa kizayuni na muungano usio na baraka wa wapenda vita wa kutaka kufuta makubaliano hayo au kuyafanyia mabadilko.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia imelaani vitisho vya Marekani vya kutaka kuwaweka Wairani wengine katika orodha ya vikwazo ya nchi hiyo  na kusema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wanachama wengine wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na jamii ya kimataifa wamesisitiza mara kwa mara kwamba, makubaliano hayo ni hati ya kimataifa na hayawezi kujadiliwa tena. 

Rais Donald Trump wa Marekani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu haitatekeleza zaidi ya majukumu yake yaliyoainishwa katika makubaliano ya JCPOA, haitakubali mabadiliko ya aina yoyote katika makubaliano hayo si sasa wana katika siku za usoni na wala haitaruhusu kufungamanishwa makubaliano hayo na maudhui nyingine yoyote. 

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia imeitaka Marekani itekeleze kikamilifu majuku yake kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.   

Tags

Maoni