Feb 09, 2018 12:55 UTC
  • Mapinduzi ya Kiislamu; umoja wa kitaifa, utukufu wa Uislamu na dola la kimataifa la Imam Mahdi (af)

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yana sifa za kipekee. Umoja wa kitaifa na utukufu wa Uislamu ambayo ni misingi muhimu ya dola la kimataifa la Imam Mahdi (af) ni baadhi ya sifa za mapinduzi hayo.

Wananchi walikuwa na nafasi muhimu na ya msingi pembeni ya kiongozi wao Imam Khomeini (MA) katika ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na hivyo kudhihirisha kwa njia ya kuvutia kabisa umoja wao wa kitaifa. Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalitoa mfano bora zaidi wa kuigwa na nchi zingine za Kiislamu kuhusu suala zima la umoja wa kitaifa. Kufuatia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, mafundisho ya Uislamu yaliimarishwa nchini Iran na umoja huo ambao unapewa umuhimu mkubwa katika dini hii tukufu. Kufuatia ushindi huo, umoja wa kitaifa na utukufu wa Uislamu ulidhihirishwa wazi katika nyanja mbalimbali nchini na suala hilo kuchukuliwa kuwa jiwe la msingi la kuasisiwa serikali ya kimataifa ya Imam Mahdi (af). Utambulisho wa Kiislamu una nafasi muhimu sana katika mkondo wa kuasisiwa serikali hiyo na bila shaka wananchi wa Iran walitoa mchango mkubwa katikamkondo huo kupitia Mapinduzi ya Kiislamu.

Uungaji mkono wa wananchi kwa Mapinduzi ya Kiislamu

Umoja wa Kitaifa na utukufu wa Uislamu ni utambulisho wa wananchi wa Iran ambao ulithibiti kupitia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ambapo hii leo makabila yote ya Iran yanaishi kwa amani chini ya mwavuli mmoja wa utambulisho huo. Ili kufikia umoja na mshikamano mbele ya ulimwengu wa kufri bila shaka ulimwengu wa Kiislamu unahitajia utambulisho halisi, kuamini utukufu wa Kiislamu na vilevile kujiamini wenyewe katika kivuli cha mafundisho ya Kiislamu. Kufuatia ushindi huo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikisisitiza kuzingatiwa nafasi ya umoja na utukufu wa Kiislamu katika ngazi za kimataifa na kuamini kuwa njia pekee ya kutatuliwa matatizo yaliyoko hivi sasa duniani ni kupitia umoja. Umoja bila shaka unaimarisha maradufu utukufu wa Kiislamu na ndio maana daima maadui wa Uislamu wakawa wanafaya juhudi za kuvuruga umoja huo kupitia njama mbalimbali katika ulimwengu wa Kiislamu ili kudhoofisha imani ya kudhihiri Imam Mahdi (af).

Kikosi cha Walinzi wa Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Hatua ya kwanza ya kufikia umoja unaokusudiwa ni kuwawezesha Waislamu watambue nguvu yao kubwa ulimwenguni na kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya kidini na wanazuoni, jambo hilo haliwezi kufikiwa ila kwa kutegemea nadharia ya Umahdi ambayo kwa hakika inawapa Waislamu bishara njema ya kufikia utukufu na heshima duniani. Kuhusiana na suala hilo Imam Khomeini (MA) anasisitiza juu ya kuhuishwa utamaduni wa Umahdawi na kusubiri kudhihiri kwa Imam Mahdi (af) kama mojawapo ya nguzo muhimu za Uislamu kwa kusema: 'Kusubiri faraja ni kusubiri nguvu ya Uislamu na tunapasa kufanya juhudi za kuthibiti nguvu ya Uislamu ulimwenguni na hivyo kuandaa uwanja wa kudhihiri Imam Mahdi (af) Inshallah.' Katika sehemu nyingine Imam Khomeini (MA) anasema: 'Mapinduzi ya watu wa Iran ni nukta ya kuanza mapinduzi makubwa ya ilimwengu wa Kiislamu kwa upeperushaji bendera wa Hadharat Hujjat, roho zetu ziwe fidia kwake.'

Upeo wa shughuli za Mapinduzi ya Kiislamu hauishii ndani ya mipaka ya Iran tu bali umeenea na kuwajumuisha Waislamu wote duniani. Kuhusu hilo Ayatullah Ali Khameni Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anasema: 'Tuna ujumbe. Iran ya Kiislamu na Muirani  Mwislamu ana ujumbe ambao ni zaidi ya maneno haya. La Hasha! Madai kuwa sisi tuna lengo la kuteka ardhi na nchi nyingine duniani, asilani, si hivyo kabisa. Hakina Mwislamu hapasi kuwa na fikra ya kuteka nchi yoyote duniani, bali suala ni la kufikisha ujumbe kwa wanadamu.'

Kiongozi Muadhamu akihutubia kikosi cha anga cha Jamhuri ya Kiislamu hivi karibuni

Hii leo umuhimu wa kuwepo umoja na utukufu wa Kiislamu umedhihirika wazi kuliko wakati mwingine wowote. Njama za kuanzisha makundi ya kigaidi na kitakfiri magharibi mwa Asia hazina lengo jingine ghairi ya kuzua mivutano na mapigano kati ya nchi za Kiislamu na hili ni suala ambalo linatekelezwa kwa shabaha ya kupotosha na kuziweka mbali nchi hizo na lengo lao kuu. Kuhusu suala hilo, Jamhuri ya Kiislamu ambayo haipuuzi wala kufumbia macho masuala muhimu yanayouhusu ulimwengu wa Kiislamu ina nafasi muhimu katika kupambana na makundi hayo ya kitakfiri ambayo yamebuniwa na maadui sugu wa ulimwengu wa Kiislamu, nafasi ambayo inatokana na uwajibikaji wake kuhusu ujumbe wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa walimwengu.

Tags

Maoni