• Khatibu: Marekani imekuwa ikipata vipigo kutoka Iran kwa miaka mingi

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran ameashiria njama za Marekani kwa lengo la kuipa pigo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema, Marekani na waitifaki wake katika miaka ya nyuma wamepata vipigo vingi kutoka Iran.

Akihutubia umati mkubwa wa waumini, Hujjatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiqui, Khatibu wa Sala ya Ijumaa wiki hii mjini Tehran ameongeza kuwa: "Marekani,Saudi Arabia na waitifaki wao wanadhani kuwa kwa kuibua kundi la kigaidi la ISIS au Daesh na kuwasilisha mipango ya kujitenga eneo la Kurdistan la Iraq, kuikalia kwa mabavu Iraq, masuala ya Lebanon sambamba na kudhoofisha mrengo wa mapambano au muqawama wanaweza kuitenga Iran lakini kwa busara wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Iran imeweza kuwapa pigo kubwa."

Hujjatul Islam wal Muslimin Siddiqui aidha ametoa pongezi kwa munasaba wa kuwadia Alfajiri 10 za kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979 na kusema, Mapinduzi ya Kiislamu yalikuwa muujiza mkubwa. Ameongeza kuwa, ustawi wa Iran katika nyuga za nyuklia, tiba, makombora, nano teknolojia na kujitosheleza katika sekta zinginezo ni kati ya mafanikio ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran ameongeza kuwa, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni chanzo cha kuwarejeshea wananchi wa Iran uhuru , izza na heshima ya watu wa Iran na kuilinda nchi ili utajiri wake usiporwe na mabeberu.

Sala ya Ijumaa Tehran 09/02/2018

Kila mwaka tarehe Mosi Februari mwaka 1979 ambyo ni siku ya kurejea Imam Khomeini MA kutoka uhamishoni, huwa ni mwanzo wa Alfajiri 10 za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

 Ushindi wa mapinduzi hayo matukufu ulipatikana siku kumi baada ya kurejea nchini Imam Khomeini MA. Hivyo Februari 1 kila mwaka ni siku ya kuanza sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.

Siku hiyo ya Februari  mamilioni ya watu walimiminika katika mitaa na barabara za mji mkuu Tehran kumpokea kiongozi wao. Sherehe hizi hufikia kileleni Februari 11 siku ya ushindi kamili wa Mapinduzi ya Kiislamu, kila mwaka ambapo wananchi hutangaza tena kufungamana kwao na malengo matukufu ya muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini MA na aliyechukua nafasi yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei.

Tags

Feb 09, 2018 14:15 UTC
Maoni