• Kiongozi: Mashia na Masuni nchini wako bega kwa bega katika vipindi vigumu kabisa

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kusimama kidete Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mbele ya ujahilia mamboleo pamoja na kuwepo vikwazo na njama zote za kijeshi na kiutamaduni za adui kunatokana na imani na kujitolea mhanga Wairani.

Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyasema hayo katika mkutano na wasimamizi wa Kongamano la Mashahidi wa Mkoa wa Sistan na Baluchistan. Kiongozi Muadhamu alitoa kauli hiyo Februari tano na ikatangazwa leo katika kongamano hilo ambalo limefanyika katika mji wa Zahedan kusini mashariki mwa Iran.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema: "Pamoja na kuwepo vipawa  vingi katika zama za tawala za Qajar na Pahlavi, watu wa Sistan na Baluchistan walikuwa wakipuuzwa na hilo lilipelekea vipawa vya watu visidhihirike."

Aidha amesema Sistan na Baluchistan sawa na mikoa ya Kurdistan na Golestan ni dhihirisho la Umoja wa Kiislamu na kigezo cha maisha ya kidugu baina ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni kwa ulimwengu. Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuhusu ulazima wa kuwa macho mbele ya njama za adui za kuibua mifarakano na kuongeza kuwa: "Kufa shahidi kijana wa Kisunni katika zama za kujihami kutakatifu au kufa shahidi mwanazuoni (maulawi) wa Ahlu Sunna wakati akiyalinda Mapinduzi ya Kiislamu mbele ya hujuma za walio dhidi ya Mapinduzi ni ishara ya udugu na kuwa bega kwa bega Shia na Sunni katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika vipindi vigumu zaidi."

Kiongozi Muadhamu akiwa na  wasimamizi wa Kongamano la Mashahidi wa Mkoa wa Sistan na Baluchistan

Kiongozi Muadhamu amesema inapasa zifanyike jitihada za kiutamaduni na kisanii ili kuweka wazi ukweli huu na kwa njia hiyo kubainisha umoja halisi.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa: "Madhihirisho kamili ya imani imara katika msururu muhimu sana wa imani na muqawama ni mashahidi na wenye kujitolea, kwa hivyo Mfumo wa Kiislamu unapaswa kuwaenzi na kuwaheshimu mashahidi.

Tags

Feb 13, 2018 16:49 UTC
Maoni