• Wairani 90,000 kutelekeza ibada ya Hija mwaka huu

Mwakilishi wa Faqihi Mtawala na Msimamizi wa Mahujaji Wairani amesema: "Mwaka huu Mahujaji Wairani katika Baitullah al Haram watakuwa ni 90,000."

Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Qadhi Asghar ameongeza kuwa: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia zimetiliana saini mapatano na kwa mujibu wa mwafaka huo, mbali na kudumishwa suhula za Mahujaji za mwaka jana, mwaka huu pia kutakuwa na huduma bora zaidi."

Mwakilishi wa Faqihi Mtawala katika masuala ya Hija na Ziara ameongeza kuwa kiwango cha hoteli za Mahujaji Wairani mwaka huu kitakuwa bora zaidi ya mwaka jana.

Mwenyekiti wa Shirika la Hija la Iran Bw. Hamid Mohammadi (kushoto) na Waziri wa Hija wa Saudia Mohammad Saleh bin Taher Benten

Kikao cha kwanza cha mazungumzo ya mwaka huu wa Hijria Qamaria kilifanyika baina ya ujumbe wa Hija wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Wizara ya Hija ya Saudi Arabia Disemba 29 mwaka 2017.

Mwenyekiti wa Shirika la Hija la Iran Bw. Hamid Mohammadi na Waziri wa Hija wa Saudia Mohammad Saleh bin Taher Benten walifanya mazungumzo kwa lengo la kuandaa ratiba ya Hija ya mwaka huu. Ujumbe wa Iran katika mazungumzo hayo ulisisitiza ulazima wa kupewa huduma bora na kudhaminiwa usalama sambamba na kuhifadhi heshima ya Mahujaji Wairani.

Tags

Feb 19, 2018 15:37 UTC
Maoni