• Utulivi kamili katika eneo la Pasdaran la Tehran baada ya ghasia

Mkuu wa Polisi katika mji mkuu wa Iran, Tehran, amesema kuna utulivu kamili katika eneo la kaskazini mwa mji huu na hakuna tatizo lolote katika eneo hilo

Kamanda wa Polisi Kanda ya Tehran, Jenerali Hussein Rahimi ametoa taarifa Jumanne alasiri kuhusu picha zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinazoonesha eti kumeibuka tena ghasia katika eneo la Pasdaran mjini Tehran na kusema: "Habari hizo ni za uongo kabisa na kuanzia Jumatatu usiku eneo hilo limeshuhudia utulivi kamili na wala hakuna tatizo lololote."

Kamanda wa Polisi Kanda ya Tehran  pia ameashiria tetesi za uwezekano wa kuibuka tena ghasia katika eneo la Pasdaran na kusema, hakuna uwezekano huo na hakuna tatizo eneo hilo.

Kwa upande wake, Msemaji wa Polisi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Brigedia Jenerali Saeed Muntadhar al Mahdi leo asubuhi amesema barabara ya Pasdaran imerejea katika hali ya kawaida baada ya watu waliohadaiwa na waliokuwa wanavuruga usalama na amani kuondolewa.

Maafisa wa usalama wakilinda doria katika barabara ya Pasdaran mjini Tehran

Katika oparesheni ya Jumatatu usiku ya maafisa wa usalama kwa lengo la kurejesha utulivu katika Barbara ya Pasdaran, maafisa watatu wa polisi na maafisa wawili wa jeshi la kujitolea la wananchi, Basiji waliuawa shahidi baada ya kugongwa na gari. Katika oparesheni hiyo maafisa kadhaa wa polisi walijeruhiwa kama ambavyo pia wahuni na waibua ghasia walijeruhiwa katika makabiliano na maafisa wa usalama.

Wahalifu hao pia walisababisha hasara kubwa katika eneo hilo ambapo magari kadhaa yaliharibiwa. Wahalifu  na wavuruga usalama walioshiriki katika ghasia hizo wanadai kuwa ni kutoka pote la kisufi  la Gunabadi.

Feb 20, 2018 15:29 UTC
Maoni