• Ayatullah Kermani: Marekani, Israel na Saudia zinahamakishwa na maendeleo ya Iran

Khatibu wa muda wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo Tehran, amesema kuwa Marekani, utawala haramu wa Israel na Saudia zimeungana kieneo na kimataifa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba zinapandwa mno na hamaki zinapoona maendeleo ya taifa hili la Kiislamu.

Ayatullah Mohammad Ali Movahhedi Kermani ameyasema hayo katika hotuba ya Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran ambapo sambamba na kuashiria maendelea ya Mapinduzi ya Kiislamu humu nchini amesema, licha ya kuweko njama mbalimbali za maadui, lakini Iran ya Kiislamu itaendelea kusonga mbele katika nyuga tofauti na kamwe haitorudi nyuma.

Saudia na Israel marafiki wakubwa

Ayatullah Movahhedi Kermani pia amelaani jinai na hivi karibuni zilizofanyika katika eneo la Pasdaran, kaskazini mwa mji wa Tehran ambazo zilipekea kuuawa shahidi askari polisi watatu na mabasiji wawili wa kikosi cha kujitolewa cha wananchi na kujeruhi wengine. Amevitaka vyombo vya mahakama kuwachukulia hatua kali wahusika wa jinai hizo.

Aidha khatibu wa muda wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo Tehran ametoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa ajali ya ndege iliyokuwa inafanya safari kati ya Tehran na mji wa Yasuj, na amewataka wafiwa kuwa na subira huku akiwaombea maghufira marehemu wa ajali hiyo.

Pande tatu hatari kwa ulimwengu wa Kiislamu duniani

Kadhalika amewapongeza viongozi wa serikali kwa ujumla kutokana na juhudi zao za kuwashughulikia wahanga wa tetemeko la ardhi mjini Kermanshah, magharibi mwa Iran ambapo pia amewataka kufanya juhudi zaidi kwa ajili ya kutatua matatizo ya watu hao.

Tags

Feb 23, 2018 15:30 UTC
Maoni