• Matarajio ya nchi wanachama wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA na majukumu ya wakala huo

Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA ni taasisi yenye kuratibu jitihada za kimataifa katika masuala ya atomiki na kutoa huduma za kitaalamu na ushauri kwa lengo la kuhimiza na kuimarisha usalama wa nyuklia katika uga wa kimataifa. Lakini swali linalojitokeza hapa ni hili, je, IAEA imeweza kutekeleza vizuri jukumu lake hili la kimsingi?

Reza Najafi mwakilishi wa Iran katika IAEA na mwenyekiti wa Kundi la 77, siku ya Jumanne, katika kikao cha msimu cha Baraza Kuu la IAEA ameutaka wakala huo wa Umoja wa Mataifa uchukue hatua za kuziunga mkono nchi wanachama katika nyuga mbali mbali za mitambo ya nyuklia na pia katika masuala yote yanayohusiana na utumiaji salama na sahihi wa teknolojia ya nyuklia.

Kwa mujibu wa hati ya IAEA, taasisi hiyo pia inapaswa kuhusika katika suala la ukaguzi wa shughuli za nyuklia mbali na kuzipa nchi wanachama teknolojia ya kisasa kabisa ya matumizi ya nyuklia kwa malengo ya amani.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama mwanachama hai wa IAEA ambaye anaheshimu vizuri ahadi zake inatarajia  kuungwa mkono na wakala huo katika teknolojia za kisasa za nyuklia.

Kwa mujibu wa mkataba wa NPT wa kuzuia kusambazwa silaha za nyuklia, IAEA ina majukumu mawili ambayo inapaswa kuyatekeleza kwa uangalifu mkubwa.

Kikao cha Bodi ya Magavana ya IAEA

Jukumu la kwanza  ni kufuatilia uangamizwaji wa silaha za nyuklia katika fremu ya mkataba NPT na kusimamia kikamilifu zoezi hilo. Jukumu la pili ni kuwa na nafasi muhimu na amilifu katika kuzisiadia nchi kustawisha teknolojia ya nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani.

Usalama wa kinyuklia pia ni kati ya ajenda muhimu za kikao cha wiki hii cha msimu cha Bodi ya Magavana wa IAEA.

Ali Mutaharinia mchambuzi wa masuala ya kimataifa katika kutathmini ushirikiano wa Iran na IAEA anasema: "Msimamo wa IAEA umekuwa wa uhakika zaidi kutokana na udiplomasia amilifu wa Iran na kwa kiasi fulani wakala huo haushinikizwi na madola makubwa. Kwa kuzingatia sera yake ya kuwa na mahusiano amilifu na yenye taathira, Iran kwa kiasi kikubwa imeweza kupunguza gharama kubwa za kitaifa katika kupata teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani."

Ali Reza Najafi, mwakilishi mkuu wa IAEA

Yukia Amano Mkurugenzi Mkuu wa IAEA katika safari yake mjini Tehran Oktoba 30 mwaka 2017 alizungumza kuhusu udharura wa kuungwa mkono miradi ya utafiti ya Iran na kuimarishwa ushirikiano wa Iran na wakala huo katika nyuga mbali mbali huku akisema kwa kusisitiza kwamba: "Naunga mkono kuteuliwa wataalamu Wairani katika nyadhifa za usimamiaji wa IAEA."

Mbali na Iran, nchi nyingi wanachama wa IAEA hasa zinazostawi zimetaka msaada wa kitaalamu wa wakala huo katika mipango yao ya nyuklia kwa malengo ya amani.

Kwa msingi huo, mwakilishi wa Iran katika IAEA, akiwa anawakilisha nchi za Kundi la G77, (Jumuiya ya nchi 77 zinazsotawi ambayo ilianzishwa mwaka 1964) amebainisha umuhimu wa makujumu ya IAEA kwa niaba ya nchi hizo.

Tags

Mar 07, 2018 10:51 UTC
Maoni