• Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mnasaba wa kuwadia mwaka mpya wa Kiirani

Taifa la Iran limeanza sherehe za mwaka mpya wa Nairuzi kwa ujumbe muhimu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ujumbe ambao una nukta muhimu zinazotia matumaini kuhusiana na mustakbali wa taifa.

Huku akitoa ujumbe wa heri na fanaka za mwaka mpya wa 1397 Hijiria Shamsia kwa taifa la Iran, na hasa kwa familia tukufu za mashahidi, waliojeruhiwa vitani na vijana wanaotia matumaini na wanaoendesha harakati za kielimu nchini, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewatakia wote mwaka mpya wenye furaha uliojaa heri na baraka na kuutaja huu kuwa ni mwaka wa kuunga mkono na kutetea bidhaa za Iran. Mwaka uliopita kwa taifa la Iran ulikuwa ni mwaka uliojaa matukio mazuri na mabaya ambapo taifa lilishuhudia matukio mengi machungu na mengine ya kutia moyo. Mahudhurio ya Wairani milioni 40 katika uchaguzi wa rais na mabaraza ya miji, ambayo yalitajwa na Kiongozi Muadhamu kuwa mahudhurio adhimu, ya kushangaza na yaliyojaa maana, ni matokeo muhimu na ya kung'ara yaliyoshuhudiwa mwaka uliopita. Mahudhurio hayo pia yalioonekana wazi katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, maandamano ya Dei 9 (Disemba 30) na vilevile ya Bahman 22 (Februari 11).

Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Ni kwa kwa kutilia maanani matukio hayo ndipo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wake kwa taifa akautaja mwaka huu kuwa ni mwaka wa kudhihiri ukubwa, nguvu na mahudhurio ya taifa na huku akiashiria mipango na njama zilizoshindwa za maadui kwa ajili ya kuzuasha vurugu na ghasia nchini katika miezi ya mwisho ya mwaka huu, akasema kwamba maandamano yasiyochochewa na yeyote ya wananchi dhidi ya wafitini yanabainisha wazi mahudhurio ya taifa kubwa, lenye mwamko, lisilozembea na lililo tayari kutekeleza majukumu katika nyanja zote la Iran.

Kwa mtazamo huo ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mnasaba wa kuwadia mwaka mpya wa Hijiria Shamsia una umuhimu mkubwa wa kistratijia. Ujumbe huo pia unasisitiza juu ya kuzingatiwa vyema fursa na vitisho vilivyoko.

Moja ya matukio ya kigaidi mjini Tehran

Maadui wa mfumo wa Kiislamu wa Iran mwaka uliopita walipanga njama nyingi zikiwemo za kuzua ghasia na machafuko ndani ya nchi na hivyo kujaribu kutoa pigo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kwa kuvuruga hali yake ya ndani. Taifa la Iran, na hata wale ambao maadui waliokusudia kutumia vibaya majina yao katika ghasia hizo walisimama imara mbele ya wachochezi hao na hivyo kwa mara nyingine kudhihirisha wazi utukufu na ukubwa wa taifa la Iran. Hivi sasa pia ambapo mwaka mpya umeanza, taifa la Iran bado limesimama imara na kwa nguvu kubwa katika nyanja zote huku likihimili vitisho na mashinikizo ya maadui. Limeamua kusonga mbele kwa nguvu zake zote ili kubadilisha vitisho hivyo kuwa fursa. Kuhusiana na suala hilo katika ujumbe wa mwaka huu wa Kiongozi Muadhamu suala la uchumi limepewa umuhimu maalumu. Huku akiutaja mwaka huu kuwa ni mwaka wa kuunga mkono na kutetea bidhaa za Iran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mara nyingine tena ameashiria umuhimu wa suala la uchumi nchini.

Maandamano ya Quds mjini Tehran

Amesema kwamba iwapo uzalishaji wa taifa utafuatiliwa kwa makini na pande zote bila shaka matatizo mengi ya kimaisha ya wananchi na suala la ajira na uwekezaji yatatatuliwa na kupunguza kwa kiwango kikubwa madhara ya kijamii. Licha ya kuwa kuna maendeleo na mafanikio makubwa ya kiuchumi yaliyopatikana nchini mwaka uliopita kupitia nara ya mwaka huo ya uchumi ngangari (wa kimapambano); uzalishaji na ajira, lakini bado kuna kazi nyingi zinazohitajika kufanyika ili kufikia kimatendo malengo ya nara hizo.

Nukta muhimu zilizobainishwa katika ujumbe wa mwaka huu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa hakika ni ramani ya njia kwa ajili ya kufikia mafanikio makubwa zaidi mwaka huu.

Tags

Mar 21, 2018 13:31 UTC
Maoni