• Kiongozi Muadhamu asisitiza juu ya mchakato endelevu na  kuzidishwa uwezo wa jeshi la Iran

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran amepongeza na kusifu utendaji na uzoefu wa thamani wa wafanyakazi wa zamani wa jeshi na huku akieleza kuwa na matarajio kuhusu mustakbali mwema wa vijana jeshini amesisitiza kuwepo mchakato endelevu na kuzidishwa uwezo wa jeshi.

Ayatullah Khamenei leo alasiri amekutana na kufanya mazungumzo na kamanda mkuu na baadhi ya makamanda wa jeshi la nchi kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kubainisha kuwa: Maendeleo yanapasa kuendelezwa ili jeshi la kesho liwe bora zaidi kuliko la leo, liwe na nguvu zaidi, lenye kuwajibika zaidi na la kimapinduzi zaidi. 

Katika mazungumzo hayo, ambayo yamejiri kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi na Wanajeshi wa Nchi Kavu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewahutubu vijana kwa kusisitiza kuwa: Kwenu nyinyi vijana azizi nataka mstafidi na ubunifu, juhudi na uwezo wenu wote wa kibinadamu kwa ajili ya kulisogeza mbele jeshi.  

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Iran aidha amepongeza misimamo ya kimapinduzi na ya umoja ya Meja Jenerali Abdulrahim Musawi Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran na kuongeza kuwa: Meja Jenerali Musawi ametoa hotuba nzuri sana kuhusu kuwa na umoja vikosi vya ulinzi; hotuba inayodhihirisha busara ya uongozi na upendo wa dhati; masuala yanayolifanya jeshi kuwa na thamani zaidi mbele ya macho ya wananchi.

Meja Jenerali Abdulrahim Musawi, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran

Tarehe 29 mwezi wa Farvardin, kwa mujibu wa kalenda ya Kiirani, ambayo ni sawa na tarehe 18 Aprili imepewa jina la Siku ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Wanajeshi wa Nchi Kavu. 

Tags

Apr 22, 2018 14:11 UTC
Maoni