• Askofu Mkuu wa Wakristo wa Iran: Imam Khomeini (MA) alikuwa daima akitilia mkazo uhuru wa jamii za dini za wachache​

Askofu Mkuu wa Wakristo wa Kiarmenia wa Tehran na kaskazini mwa Iran amesema: Imam Khomeini (MA) mwasisi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikuwa daima akitilia mkazo uhuru wa jamii za dini za wachache.

Askofu Sebuh Sarkisian, ametoa salamu za rambirambi kwa mnasaba wa kuwadia hauli ya Imam Khomeini (MA) na kuongeza kuwa: mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikuwa kila mara akisisitiza juu ya uhuru wa nembo na desturi za kidini na kijamii za jamii za dini za wachache.

Leo Jumatatu tarehe 14 Khordad mwaka 1397 Hijria Shamsia inayosadifiana na tarehe 19 Ramadhani 1439 Hijria Qamaria na tarehe 4 Juni 2018 inasadifiana na kutimia mwaka 30 tangu alipofariki dunia Imam Khomeini (MA), mwasisi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Imam Khomeini, Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Askofu Mkuu wa Wakristo wa Kiarmenia wa Tehran na kaskazini mwa Iran amebainisha kuwa: kuwepo jamii za dini za wachache kunawezesha kupatikana mchanganyiko wa kiutamaduni na kijamii katika kila nchi; na kuwepo anuai za tamaduni na jamii ni miongoni mwa sifa za wazi za aghalabu ya nchi duniani; na kwa baraka za Jamhuri ya Kiislamu wafuasi wa dini za tauhidi nchini Iran wako huru kutekeleza hafla, sikukuu na desturi za dini zao.../

Tags

Jun 04, 2018 04:14 UTC
Maoni