• Iran yalaani jaribio la mauaji dhidi ya Rais wa Zimbabwe

Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali jaribio lililofeli la mauaji dhidi ya Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa katika mji wa Bulawayo jana Jumamosi.

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumapili, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran, Bahram Qassemi sanjari na kuwatakia afueni ya haraka waliojeruhiwa katika shambulizi hilo, amekosoa vikali utumiaji wa ghasia katika mchakato wa kisiasa.

Amewaasa wananchi wa Zimbabwe kuwa macho na kuimarisha umoja wao, ili kuruhusu uchaguzi ujao nchini humo ufanyike katika mazingira ya amani na usalama.

Kwa mujibu wa David Parirenyatwa, Waziri wa Afya wa Zimbabwe, watu 15 walijeruhiwa, watatu kati yao wakiwa katika hali mbaya, baada ya kujiri mlipuko karibu na kujwaa alikokuwa ameketi Mnangagwa katika Uwanja wa White City katika mji wa Bulawayo.

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe

Mlipuko huo ulitokea wakati rais huyo wa Zimbabwe akiondoka uwanjani hapo, baada ya kuwahutubia wafuasi wake, kuelekea uchaguzi mkuu wa Julai 30.

Rais Emmerson Mnangagwa amelitaja shambulizi hilo kama la kiwoga na kusisitiza kuwa mbinu hizo katu hazitafuta azma yake ya kuwania urais na kuwahudumia wananchi wa nchi hiyo maskini ya Kiafrika.

Tags

Jun 24, 2018 07:33 UTC
Maoni