Jul 11, 2018 07:36 UTC
  • Ayatullah Khatami: Iran haitalegeza msimamo kuhusiana na kadhia ya Palestina

Msemaji wa Baraza la Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran haitalegeza msimamo wake kuhusiana na kadhia ya Palestina.

Ayatullah Ahmad Khatami amesema hayo akiwa katika mji wa Borujen katika mkoa wa Chaharmahal Bakhtiari magharibi mwa Iran na kusisitiza kwamba, Iran katu haitalegeza msimamo wake hata kidogo kuhusiana na kkadhia ya Palestina. 

Msemaji wa Baraza la Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Irna itaendelea kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina.

Ayatullah Khatami ambaye pia ni khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran ameashiria pia uuungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon na kusema kwamba, himaya na uungaji mkono kwa Hizbullah ni sehemu ya usalama wa Iran.

Imam Ruhullah Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Jamhuri ya Kiislamuu ya Iran, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon na muqawama wa wananchi wa Palestina ni mihimili mitatu ambayo imekuwa na nafasi muhimu katika kukabiliana na njama za kila siku za mhimili wa pande tatu wa Marekani, Saudi Arabi na utawala ghasibu wa Israel.

Ikumbukwe kuwa, Iran imekuwa muungaji mkono mkuu wa taifa madhulumu la Palestina tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979 kwa uongozi wa Imam Ruhullah Khomeini (Rahmatullahi Aleih).

Maoni