Jul 11, 2018 08:13 UTC
  • Dakta Kharrazi: Vitendo vya kibabe vya Marekani vimesababisha ukosefu wa usalama Mashariki ya Kati

Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Uhusiano wa Nje wa Iran amesema kuwa, uingiliaji wa madola ya kigeni katika masuala ya ndani ya nchi nyingine na miamala ya kibabe ya Marekani na utawala haramu wa Israel kuhusiana na Wapalestina ni mambo muhimu ambayo yamechangia mno kukosekana amani na uthabiti katika eneo la magharibi mwa Asia (Mashariki ya Kati)

Sayyid Kamal Kharrazi Waziri wa zamani wa Mashauuri ya Kigeni wa Iran ambaye yuko safarini nchini Ujerumani amesema katika mazungumzo yake na Norbert Röttgen, Mkuu wa Kamisheni ya Siasa za Kigeni ya Ujerumani na kuongeza kuwa, Iran imekuwa na nafasi muhimu mno katika kuleta amani na uthabiti Mashariki ya Kati.

Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Uhusiano wa Nje wa Iran  amesema bayana kwamba, mataifa ya eneo hili pia yanapaswa kufanya mazungumzo baina yao na kuleta amani na uthabiti wa eneo hili bila ya kuingiliwa na madola ya kigeni. 

Rais Donald Trump wa Marekani

Dakta Kamal Kharrazi ameongeza kuuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kufanya mazungumzo na nchi za eneo na kwamba, endapo kutakuwa na irada sahihi na ya kweli mazungumzo hayo yanaweza kuwa na natija.

Kwa upande wake Norbert Röttgen, Mkuu wa Kamisheni ya Siasa za Kigeni ya Ujerumani ameashiria migogoro na matukio ya Mashariki ya Kati na kusema kuwa, hakuna wakati ambao eneo hili lilikabiliwa na machafuko kama ilivyo hii leo, hivyo kuna haja na udharura wa nchi za eneo hili kuchukua hatua za maana ili kudhibiti hali hii. 

Tags

Maoni