Jul 12, 2018 15:01 UTC
  • Rais Rouhani amtumia ujumbe mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni

Mjumbe maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemkabidhi Rais Yoweri Museveni wa Uganda ujumbe wa maandishi kutoka kwa mwenzake wa Iran.

Baada ya kukutana na Rais Museveni wa Uganda, Murtadha Sarmadi amebainisha hatua za upande mmoja za Marekani na taathira zake mbaya kwa amani na usalama wa kimataifa na kutoa wito kwa nchi huru na zinazojitawala kuchukua msimamo mmoja wa kukabiliana na siasa na misimamo hiyo isiyo na kimantiki.

Mjumbe maalumu wa Rais wa Iran nchini Uganda amesema hatua zinazochukuliwa na Rais Donald Trump wa Marekani hususan kujiondoa nchi hiyo katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na kusema: Kuna matarajio kwamba nchi nyingine zilizotia saini makubaliano hayo zitapendekeza kifurushi kamili na cha pande zote kwa Iran na kuidhaminia maslahi yake katika makubaliano hayo.

Kwa upande wake, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda amesema nchi yake ilikaribisha na kuunga mkono makubaliano ya nyuklia ya Iran na nchi za kundi la 5+1 na kuongeza kuwa, anatarajia kwamba pande zote husika zitafanya jitihada za kulinda makubaliano hayo.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda

Rais wa Uganda wamesema kuwa, siasa na sera za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja za Marekani hazikubaliki na ametilia mkazo udharura wa kufanyika juhudi shirikishi kati ya nchi zote zinazojitawala hususan nchi zenye nguvu kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

Rais Museveni amesema Uganda iko tayari kwa ajili ya kuimarisha na kupanua ushirikiano wake na Iran katika nyanja zote.  

Tags

Maoni