• Iran yalaani hatua ya Bunge la Israel ya kutambuliwa Israel kama 'dola la Mayahudi pekee'

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamuu ya Iran amelaani vikali hatua ya Bunge la utawala haramu wa Israel (Knesset) ya kupasisha muswada wa sheria inayotaka kutambuliwa Israel kama 'dola la Mayahudi pekee'.

Bahram Qassemi  amesisitiza kuwa, ubaguzi "Apartheid" umekuwa ukkiendelea Palestina inayokaliwa kwa mabavu lakini hima na juhudi za wanamuqawama wa taifa la Palestina ubaguzi huo utahitimishwa.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri yay Kigeni ya Iran amesema bayana kwamba, utawala haramu na wa kibaguzi wa Israel umeundwa kwa msingi wa kuikalia kwa mabavu Palestina na kuwaua kwa umati wamiliki wa asili wa ardhi hiyo na katika kipindi chote cha miaka 70 utawala huo umeendelea kufanya ubaguzi.

Bunge la Israel (Knesset)

Kwa mujibu wa sheria hiyo iliyopasishwa na Bunge la Israel hapo juzi, ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo (Israel) zinachukuliwa kuwa ni za Mayahudi pekee na kwamba Wapalestina wanaoishi katika ardhi hizo watanyimwa haki zote za kiraia na za kibinadamu.

Vilevile lugha ya Kiibrania ndiyo itakayokuwa lugha rasmi katika ardhi hizo. Sheria hiyo licha ya kuutambua mji mtakatifu wa Quds kuwa eti ni mji mkuu wa utawala huo ghasibu, inatambua ujenzi na kupanuliwa kwa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi kuwa thamani ya kitaifa na kutaka hatua za haraka zichukuliwe kwa lengo la kuimarisha vitongoji vilivyopo sasa na kujengwa vingine vipya.

Jul 21, 2018 04:10 UTC
Maoni