Jul 30, 2018 07:49 UTC
  • Zarif: Marekani imepatwa na uraibu wa kuweka vikwazo

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema Marekani imepatwa na uraibu wa kuweka vikwazo dhidi ya nchi mbalimbali na kwamba Wairani watavuka kipindi kigumu cha sasa kwa umoja na mshikamano wao.

Muhammad Javad Zarif amekiambia kikao cha mabalozi na wawakilishi wa Iran nje ya nchi kwamba, historia ya mahusiano ya kigeni ya Marekani inaonyesha kuwa nchi hiyo imeweka vikwazo dhidi ya nchi nyingi, na kwamba Wairani watatumia vikwao vya Marekani kama fursa ya kuboresha uzalisha wa ndani na uuzaji nje bidhaa zisizo za mafuta. 

Dakta Zarif amesisitiza kuwa, sasa ni zamu ya nchi za Ulaya kuchagua moja kati ya kudhamini malahi ya Marekani na Donald Trump au maslahi na manufaa yao wenyewe.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema ulimwengu umefikia hitimisho kwamba Marekani inahitaji kuacha uraibu wa vikwazo. Amesisitiza kuwa taifa la Iran litawaonesha walimwengu kwamba ni kubwa zaidi ya hao wanaoliwekea vikwazo. 

Vilevile amekosoa utegemezi wa baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati kwa Marekani katika masuala ya kiusalama na kisiasa.

Tags

Maoni