Aug 05, 2018 15:42 UTC
  • Iran yalaani jaribio la kutaka kumuua Rais wa Venezuela + Video

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali jaribio la kutaka kumuua rais wa Venezeula Nicolas Maduro.

Katika taarifa yake, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram Qassemi ameashiria jaribio la kuuawa Rais Maduro huko Venezuela na kusema: "Iran inalaani kitendo hicho ambacho kimelenga kuvuruga utulivu na usalama wa Venezuela kwa maslahi ya maadui wa serikali na wananchi."

Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

 

Mapema Jumapili  Maduro alinusurika katika jaribio la mauaji lililofanywa kwa kutumia ndege zisizo na rubani (drone).

Jaribio hilo limefanyika wakati Rais wa Venezuela alipokuwa akitoa hotuba katika kambi ya jeshi mjini Caracas.

Baada ya kunusurika kuuawa, Maduro amesema kuwa Marekani na Colombia ndizo zilizofanya jaribio la kutaka kumuua. Amesema "Ilikuwa hujuma ya kutaka kuniua na Marekani pamoja na Colombia zimehusika."

 

Amesema kuwa vyombo husika vimeanza uchunguzi mara moja na kwamba watu kadhaa wameshatiwa nguvuni kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi.

Rais wa Venezuela amesisitiza kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa watu waliopanga jaribio la kutaka kumuua wanaishi Florida nchini Marekani na ameitaka serikali ya Donald Trump wa Marekani kusaidia uchunguzi huo. 

Tags

Maoni